Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amevikumbusha Vyuo Vikuu Viliyopo nchini Umuhimu wa kujikita katika Kufanya Tafiti ambazo zitatoa Ufunbuzi wa Changamoto za Kijamii na kuzisambaza kwa Watumiaji.Rais Dk, Mwinyi ametoa tamko hilo katika Mahafali ya 24 ya Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al Sumait Chukwani Wilaya ya Magahribi B,Mkoa wa Mjini Magharibi.

Dk,Mwinyi ametoa Wito kwa Viongozi wa Vyuo Vikuu kuendelea Kujenga Uwezo wa kufanya Tafiti kwa Wafanyakazi kwa kutumia Fursa ziliyopo pamoja na Kushirikiana na Vyuo Vikuu vya vyengine vyenye Wataalamu Waliobobea katika Tafiti kwa ajili ya kuwajengea Uwezo Wataalamu Wazalendo.Aidha Amesisitiza Umuhimu wa kusamabaza Matokeo ya Tafiti kwa Watumiaji kwani bila ya Kuyasambaza kwa Watumiaji ni kupoteza Rasilimali.

Rais Dk, Mwinyi amefahamisha kuwa Kutosambazwa kwa Tafiti Kunapunguza hadhi za Vyuo Vikuu kama Vitovu vya kuleta Mabadiliko ya kijamii na kutoa Rai kwa Vyuo Vikuu kuandaa Mpango Maalum Utakaohakikisha Matokeo ya Tafiti yanawafikia Watumiaji.Rais Dk, Mwinyi ameeleza kuwa ni Muhimu kwa Wizara na Idara za Serikali kushirikiana na Vyuo Vikuu kufanya Tafiti na kutumia Tafiti mbalimbali kuleta Maendeleo katika Nyanja za kijamii,Kiuchumi na Kiutamaduni.Rais Dk, Mwinyi amesema Serikali inathamini juhudi za Chuo Kikuu cha Abdulrahnan Al Sumait katika Utoaji wa Elimu kwani kunachangia Nguvu kazi na Ongezeko la Waatalamu Wazalendo katika Sekta Mbalimbali za Umma na Kijamii.

Rais Dk , Mwinyi ameupongeza Uongozi wa Chuo hicho kwa kuwa na lengo la Kuanzisha Programu Mpya Chuoni hapo Ikiwemo Shahada ya Uzamili katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Shahada ya Uzamili katika Sayansi na Ushauri Nasaha ambazo zitaakisi Mahitaji ya Taifa na zitakazoendana na Kasi ya Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia Duniani.Rais ameahidi Serikali Kuendelea kutoa Ushirikiano wa kiwango cha juu ili Chuo hicho Kifikie malengo ya Kuanzishwa kwake. 

Wahitimu 304 katika fani mbalimbali wamehitimu Katika Mwaka wa Masomo 2023-2024 ,Wanawake wakiwa 203 na 101 Wanaume, na kufikisha Wahitimu 4,993 waliohitimu katika Chuo hicho tangu Kuanzishwa kwake Mwaka 1998.