HUSSEIN MWINYI:TUJIANDIKISHE TUPIGE KURA,CCM ISHINDE KWA KISHINDO.
Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Hussein Ali Mwinyi amepokewa na Mamia ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, Viongozi na Wananchi alipowasili Zanzibar akitokea Dodoma alipoteuliwa Kupeperusha Bendera ya Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu Ujao katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Uliofanyika hivi Karibuni.
Mgombea Mteule Dk. Mwinyi alipokelewa na Mamia ya Wana CCM, pamoja na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi, Serikali , Vyombo vya ulinzi na usalama na Dini.Mamia ya Wananchi wa Zanzibar na Wana CCM walijitokeza kwa Wingi Pembezoni mwa Barabara kuu ya Uwanja wa Ndege- Kilimani kumpokea Dk ,Mwinyi aliyekuwa katika Gari la Wazi akiwapungia Mkono hadi Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi alizuru Kaburi la alieyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume na Kuweka Shada la Maua pamoja na Kuzungumza na Wazee wa Chama cha Mapinduzi na Kumpongeza pamoja na kumtakia Kila la Heri katika safari yake ya Kinyang’anyiro cha Urais wa Zanzibar.
Akizungumza na Wana CCM na Wananchi Uwanja wa Mapinduzi Square, Michenzani Dk. Mwinyi ameeleza kuwa CCM imemaliza kazi ndani ya Chama ya Kufanya Maamuzi sahihi ya kupata Wagombea wake na kazi iliobaki ni ya kutafuta ushindi wa kishindo Mwezi wa Oktoba katika Uchaguzi Mkuu.
Dk.Mwinyi amekishukuru Chama Cha Mapinduzi Kupitia ngazi zote kwa kuthamini Kazi ya Utekelezaji wa Ilani iliyofanywa naye pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuwateua tena kuwa Wagombea wa Chama hicho.Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Wana CCM na Wananchi kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura litakapoanza Mwezi Februari Mwaka huu
na hatimaye kujitokeza kupiga Kura Mwezi Oktoba ili Chama Cha Mapinduzi kipate ushindi wa kishindo.Aidha amewasisitiza kuendelea Kutunza Amani na Utulivu wa Nchi Hususani Wakati huu wa Kuelekea Uchaguzi Mkuu.