Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amesema maradhi yasioambukiza ni tatizo linalokuwa na linalohitaji ushirikiano wa taasisi za ndani ya nchi na kimataifa katika kulipatia njia Bora za kukabiliana nalo.Rais Dk, Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na timu ya Madaktari bingwa na Wataalamu wa Maradhi yasioambukiza kutoka Geneva waliofika Ikulu kuonana na naye tarehe 12 Novemba 2024.

Rais Dk,Mwinyi amefahamisha kuwa Zanzibar kama zilivo nchi nyengine duniani imekuwa na wagonjwa wa wengi wa Maradhi yasioambukiza wanaoongezeka kila mwaka hivyo inahitaji kuungwa mkono katika juhudi zake za kudhibiti ongezeko la wagonjwa wa aina hiyo.Rais Dk, Mwinyi amebainisha kuwa Zanzibar inabeba mzigo mkubwa wa Usafirishaji wa Wagonjwa kwenda nje ya nchi kutibiwa magonjwa mbalimbali ikwemo saratani hivyo suala la kujengewa uwezo Wafanyakazi wa sekta ya afya ni la umuhimu mkubwa.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amesisitiza kwa Wizara ya afya kuendelea na mchakato wa mazungumzo na timu hiyo ya Madaktari bingwa kwa dhamira ya kutafuta njia Bora utaalamu na upatikanaji wa dawa za kutibu Maradhi yasioambukiza
Rais Dk, Mwinyi amewahakikishia Madaktari bingwa hao kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana nao na kufanya kazi bega kwa bega kufanikisha lengo Lao la kuja nchini kubaini changamoto na maeneo ya Ushirikiano katika Sekta ya afya.