Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar Ina Kila sababu ya Kuimarisha Ushirikiano na Cuba kutokana na Mchango unaotolewa na Nchi Hiyo kwa Maendeleo ya Zanzibar.Rais Dkt, Mwinyi ametoa Tamko hilo alipozungumza na Rais wa Baraza la Taifa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Cuba Esteban Lazo Hernandez na Ujumbe wake Waliofika Ikulu Kuonana Naye.
Amefahamisha kuwa Uhusiano wa Muda mrefu baina ya Tanzania na Cuba ulioasisiwa na Viongozi Waasisi wa Mataifa hayo mawili ni nguzo Muhimu ya Ushirikiano inayopaswa kuendelezwa hivi sasa kwa ajili ya Maendeleo na maslahi ya Wananchi wa Pande zote mbili.Rais Dkt, Mwinyi ameishukuru Cuba kwa Misaada inayoendelea kuitoa kwa Zanzibar kwani imekua ikichangia kwa Kiasi kikubwa Maendeleo katika Sekta tofauti Hususan Sekta ya Afya na Kuimarisha Ustawi wa Wananchi wa Zanzibar.
Ameeleza kuwa Misaada ya Sekta ya Afya ikiwemo Madaktari ,Wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA),Dawa ,Vifaa Tiba na Teknolojia imekuwa Chachu ya Mabadiliko ya Sekta ya Afya hapa nchini na kuitaka Kuendelea na Misaada Hiyo.Rais Dkt, Mwinyi amesema Ujio wa Ujumbe huo ni fursa Muhimu ya kufungua maeneo Mengine ya Ushirikiano ikiwemo Uchumi wa Buluu, Elimu, Utalii , Teknolojia ,Utamaduni ,Michezo .
Ameuhakikishia Ujumbe huo kuwa Zanzibar itaendelea kuchukua kila juhudi Kuhakikisha Ushirikiano huo unaimarika zaidi na kuwa tayari kuondoa Vikwazo kwa dhamira ya Kufikia malengo ya Ushirikiano Uliopo.Rais Dkt , Mwinyi ametumia fursa Hiyo kuishukuru Cuba kwa Mchango wake ilioutoa wakati wa Mapambano ya Uhuru kwa Nchi nyingi za Afrika.
Naye Rais wa Baraza la Taifa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Cuba Esteban Lazo Hernandez ameihakikishia Zanzibar Kuendelea na Ushirikiano na Kupongeza Mabadiliko Makubwa yaliofikiwa na Zanzibar Katika Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Miundonbinu ya Barabara, Hospitali na Vituo vya Afya hapa nchini.Ameeleza kuwa Ushirikiano wa Nchi hizo katika Mapambano ya kutafuta Uhuru sasa ni lazima uelekezwe katika Kuleta Maendeleo ya kiuchumi na Kuimarisha Maisha ya Wananchi wa Pande zote mbili.