RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema ujenzi wa mindombinu ya elimu nchini unalengo la kuboresa sekta ya elimu iliyoko kwenye mageuzi makubwa ya maendeleo.Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipofungua skuli ya Sekondari Hassan Khamis Hafidhi iliopo Mtopepo, Shehiya ya Munduli Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa mjini Mgharibi, ikiwa ni mwendelezo wa shamrashamra za maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi amesema, nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kupunguza msongamano wa wanafunzi wengi madarasani na kubakisha wastani wa wanafunzi 45 kwa kila darasa moja, sambamba na kuweka mkondo mmoja kwa skuli zote za Unguja na Pemba.Dk. Mwinyi pia alisema hali hiyo itasaidia matokeo mazuri kwa kuwepo mazingira mazuri ya kujifunzia.
Akizungumzia mafanikio makubwa yanayoendelea kupatikana kwenye sekta ya elimu, Rais Dk. Mwinyi ameeleza Sekta hiyo imevuka malengo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM 2021/ 2025 kwa kuboresha miundombinu ya kisasa, zikiwemo Makataba, madarasa yenye ubora wa hali ya juu, maabara madawati, kuboeshwa kwa maslahi ya walimu sambamba na kuongeza ajira za walimu wa hesababati na sayansi, Unguja na Pemba.
Aidha, Rais Dk. Mwiniyi aliushukuru uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa kufanikisha vyema miradi yote za Serikali inayosimamiwa na Wizara hiyo kwa kuifanikisha kwa mafanikio makubwa.Alisema, mradi wa Skuli ya Hassan Khamis Hafidh licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa wakati wa utekelezaji wake hatimae, umefanikishwa kwa mafanikio makubwa nakuongeza kuwa ni mradi pekee uliotekelezwa kwa fedha za uviko 19 kukawia kuzinduliwa hatimae umekamilika ukiwana mafaniko makubwa.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa skuli hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Muhamed Mussa, ameiahidi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuisimamia kwa ufanisi wa hali ya juu miradi yote inayotekelewa na kusimamiwa na Wizara hiyo.Pia, Waziri Lela, amemshukuru Rais Dk. Mwinyi na Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa weledi wao wa kuendelea kuusimamia na kuudumisha Muungano wa Tanzania ambao kwasasa unatimiza miaka 60 tokea kuasisiswa kwake mwaka 1964.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khamis Abdalla alisema ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Hassan Khamis Hafidh wa ghorofa tatu ulinza mwezi Februari mwaka 2022 hadi uliposuasua mwezi wanane mwaka huo na baadae kukabidhiwa Chuo cha mafunzo kwaajili ya kuuendeleza hadi kukamilika kwake.Aidha, Katibu huyo amesema ujenzi wa skuli hiyo umejumuisha madarasa 41, ofisi nne za walimu, ofisi ya mwalimu mkuu, vyoo 52, maktaba, maabara, chumba cha kompyuta na stoo, na ukumbi mkubwa wa mikutano.
Akizungumza kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Magharibi kichama, Muhamed Rajab Sudi alisifia uongozi wa Rais Dk. Mwinyi na kuuelezea sio uongozi wa kujionesha bali ni wakuwatumikia wananchi kwa vitendo kama ambavyo mageuzi makubwa ya maendeleo yanavyoonekana nchi nzima chini ya kipindi kifupi cha uongozi wake.