Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ameialika Timu ya   Taifa ya Zanzibar, ZANZIBAR HEROES Ikulu kwa Chakula cha Mchana Siku Ya Jumatano tarehe 15 Januari 2025.Rais Dk.Mwinyi ametoa Mwaliko huo Uwanja wa Gombani Pemba baada ya Timu hiyo kufanikiwa Kulitwaa Kombe la Michuano ya Mapinduzi 2025.

ZANZIBAR HEROES imeifunga Timu ya Taifa ya Burkinafaso kwa Magoli 2-1 katika Mchezo Mkali wa Fainali uliochezwa Uwanja wa Gombani Mgeni Rasmi akiwa Rais Dk.Mwinyi ambae   alikabidhi Kombe kwa bingwa Wa Michuano hiyo ZANZIBAR HEROES .

ZANZIBAR HEROES ilitinga Fainali badaa ya Kuilaza Timu ya Taifa Ya Kenya HARAMBE STARS
Kwa goli 1-0. Mbali na Kombe la Ubingwa Timu hiyo pia imejinyakulia kitita Cha Shilingi Milioni 100.