Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amepongeza uamuzi wa Benki ya Stanbinc Tanzania wa kuwa na Tawi Zanzibar kwani kutaongeza idadi ya Benki na kurahisisha huduma kwa wananchi.Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Uongozi wa Benki ya Stanbic Tanzania ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Patrick Rutabanzikwa waliofika Ikulu Zanzibar tarehe 13 Novemba 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amefahamisha kuwa ukuaji wa kasi wa Uchumi unaoendelea hivi sasa unahitaji kuwepo na mchango wa taasisi makini za kifedha .Naye Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo Patrick Rutabanzikwa ameeleza kuwa maendeleo yanayoonekana Zanzibar hivi sasa na ongezeko la mahitaji ya taasisi za kibenki kwa wananchi kumechochea kwa Stanbic kufungua Tawi lake.

Benki ya Stanbic itajenga Tawi hilo katika Mtaa wa Biashara wa Mlandege na inatarajia kutumia kiasi cha Shillingi Milioni Mia nane kukamilisha Ujenzi huo.