Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi amesema hakuna Maendeleo Endelevu na ya Haraka endapo Wanawake hawatashirikishwa na kuwezeshwa Ipasavyo Kiuchumi.Mama Mariam Mwinyi ambae pia ni Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation ametoa Tamko hilo alipozungumza na timu ya Watendaji wa Shirika la Action Aid Tanzania Waliofika Afisini kwake Migombani Kuonana Naye.

Mama Mariam ameeleza kuwa bado kuna Kazi kubwa ya kufanya inayohitaji Ushirikiano wa Taasisi hizo mbili Ili kuwainua Wanawake Kiuchumi Hususani Wakulima wa zao la Mwani.Ameeulezea Ujumbe huo kuwa licha ya Wakulima wa Mwani kutumia nguvu kubwa bado hawajanufaika na zao Hilo na kuishauri Action Aid Tanzania kwa pamoja na ZMBF kulipatia Suluhusho tatizo Hilo.

Ameainisha Eneo jengine la Ushirikiano kuwa ni Mapambano dhidi ya Vitendo vya Udhalilishaji wa Jinsia wanavyofanyiwa Wanawake na Watoto alilosema linahitaji kuwa na Mkakati Maalum wa kuwajengea Uwezo wa kupaza sauti zao na kutambua Halki zao za Msingi.

Mama Mariam Mwinyi amefahamisha kuwa Tatizo la Muhali bado mi Tatizo kubwa linaloikabili Zanzibar Katika Juhudi za kukabiliana na Vitendo vya Udhalilishaji.” Ninatamani kuona Watoto wote wanafundishwa kujua haki zao ili kuwalinda na Udhalilishaji” alisisitiza Mama Mariam. 

Akizungumza Mradi wa Maj Safi na Salama kwa Wanafunzi uliowasilishwa na Action Aid katika Kikao Kazi hicho amesema ni Mradi Muhimu utakaowahakikishia Wanafunzi Upatikanaji wa maji Salama wakiwa Skuli pamoja na kuwalinda na Magonjwa yanayotokana na matumizi ya maji yasio salama

Ameihakikishia Action Aid Tanzania kuwa Zanzibar Maisha Bora Foundation iko tayari kushirikiana nao kufanya Kazi kwa Ukaribu zaidi kuyafikia Matarajio na Malengo ya Taasisi hizo ambayo yanafanana.

Naye Mshauri Muelekezi wa Action Aid Tanzania kutoka FANA CONSULTING Oscar Mukassa amekielezea Kikao hicho kuwa kimefungua Milango ya Ushirikiano na ZMBF hasa Maeneo Muhimu ya Kuwajengea Uwezo Wanawake Kushiriki katika Uchumi, Kuliongezea Mnyororo wa thamani zao La Mwani na Mradi wa Maji Safi na Salama kwa Wanafunzi wakiwa Skuli na Mapambano dhidi ya Vitendo vya Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto.

Meneja wa Miradi wa Zanzibar Maisha Bora Foundation Joseph Kaphipa amesema Kikao hicho ni kimetoa fursa Muhimu ya Kuwa na Washirika wa kuunga mkono Juhudi za Taasisi Hiyo za kuleta Mabadiliko ,Kuwajengea Uwezo Wanawake , Kuondoa Tatizo la Ukosefu wa lishe kwa Mama na Mtoto,,kuliinua zao la Mwani pamoja na Utafutaji wa Masoko ya ndani na nje ya Nchi.