Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amesema Miaka 61 ya Mapinduzi ni Kumbukumbu ya Wananchi wa Zanzibar kujikomboa Kiuchumi ,Kisiasa na Kijamiì yaliyotokana na Madhila ya kutawaliwa.Rais Dk,Mwinyi Ametoa Tamko hilo alipowahutubia Maeflu ya Wananchi katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Uwanja Wa Gombani,Pemba.

Ameeleza kuwa Mafanikio Makubwa yamepatikana katika kufikia Malengo ya Mapinduzi ya Usawa, Wananchi kuwa Wanufaika wa Rasilimali na fursa sawa bila ya Upendeleo.Rais Dk, Mwinyi amebainisha kuwa Serikali imeitafsiri dhana ya Mapinduzi kwa Kuleta Mageuzi ya Kiuchumi ,Kisiasa na Kijamii.Aidha ameeleza kuwa Nchi imepata Mafanikio Makubwa katika kukuza Uchumi, Kuongeza Ukusanyaji wa Mapato na kudhibiti Matumizi yote.

Eneo jengine ambalo Dk ,Mwinyi amelielezea kuwa la Mafanikio ni Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi Kuimarisha Miundombinu ya Barabara , Viwanja vya Ndege,Bandari, Nyumba za Makaazi ,Miundombinu ya Michezo, Huduma za Afya ,Umeme Elimu na Kuimarisha Demokrasia na Utawala Bora.

Rais Dk, Mwinyi ametoa wito kwa Wananchi kufanya Kazi kwa Bidii Uadilifu ,Umahiri na Uzalendo kwa kuweka Mbele Maslahi ya Nchi kama Walivyofanya Waasisi wa Taifa.Aidha Amewasisitiza Wanasiasa ,Viongozi wa Dini na Wananchi kuwa Mstari wa mbele katika kudumisha Amani na Utulivu wa nchi   ili Maendeleo Makubwa zaidi yapatikane.

Akizungumzia suala la Uchaguzi Dk,Mwinyi amesema ni wajibu wa kila Mwananchi Kuiombea Nchi Amani na Utulivu na Mshikamano ili hatimae Nchi ifanye Uchaguzi wa Kidemokrasia,Uwazi na Misingi ya Kisheria.Maadhimisho hayo ya Miaka 61 ya Mapinduzi pia yalihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassan.

Gwaride Rasmi la Vikosi vya Ulinzi na Usalama liliyapamba Maadhimisho hayo ambayo pia yaliambatana Na Maandamano ya Wananchi wa Mikoa Mitano ya Zanzibar pamoja na Onesho la Makomandoo wa Jeshi la Wanachi wa Tanzania (JWTŹ)