Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar pia Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwapungia mkono wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Mikoa ya Pemba waliofika kumlaki katika maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Chake chake Pemba leo alipofika kuwashukuru Wananchi na wanaCCM kisiwani humo kwa kuchaguliwa kwake katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa 10, kushika nafasi hiyo ya juu katika Chama cha Mapinduzi CCM.