Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Wananchi katika Mazishi ya Marehemu Muhammad Ibrahim Sanya yaliofanyika Leo.Rais Dkt,Mwinyi aliwaongoza Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Maiti katika Msikiti Jibril Mkunazini, Wilaya ya Mjini.

Marehemu Ibrahim Sanya amefariki Jana wakati akitibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Wa Mjini Magharibi Lumumba.Wakati wa Uhai wake Marehemu Ibrahim Sanya aliwahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Jimbo la Mkunazini kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF).

Marehemu Sanya amezikwa Eneo la Makaburi ya Kijitoupele,Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.