Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewahakikishia Wananchi wa Mpapa kuwa Serikali itazifanyia Kazi Changamoto za Kijamii ziliomo katika kijiji hicho.Alhaji Dkt, Mwinyi ametoa Tamko hilo alipotoa Salamu kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya Kujumuika katika Sala ya Ijumaa, Msikiti wa Ijumaa Mpapa, Wilaya ya Kati ,Mkoa wa Kusini Unguja.
Changamoto hizo zilizobainishwa na Wananchi ni Uchakavu wa Barabara za ndani , Ukosefu wa Uzio katika Skuli ya Mpapa na Ukosefu wa huduma za Karibu za Afya kutokana na kutomalizika kwa Kituo cha Afya kiliopo kwa Miaka mingi ambacho kimejengwa kwa nguvu za Wananchi.Rais Dkt, Mwinyi amewahakikishia kuwa Serikali itamaliza Changamoto hizo alizoziielezea kuwa ni za Muhimu.
Alhaj Dkt, Mwinyi amewasisitiza Waumini hao Kuendelea kuiombea Nchi Amani wakati huu ikielekea katika Uchaguzi Mkuu pamoja na Viongozi Wakuu wa Nchi.Amefahamisha kuwa Maendeleo yanayofikiwa hivi sasa hapa nchini yanatokana na kuwepo kwa Amani na kuahidi Kuendeleza Juhudi za kuleta Maendeleo Zaidi.
Wakati huohuo Rais Dkt, Mwinyi alikikagua Kituo hicho cha Afya ambacho hakijamalizika kwa takribani Miaka 30 tangu kilipojengwa.