Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika Nyanja mbalimbali za Maendeleo kwani ni Mshirika Muhimu katika Juhudi za kukuza Uchumi.Rais Dkt,Mwinyi ametoa Tamko hilo alipofungua Kongamano la Biashara la Zanzibar na Ulaya ,Hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege,Wilaya ya Mjini.
Rais Dkt , Mwinyi ameuhakikishia Umoja wa Ulaya kuwa Serikali inachukua Juhudi maalum Kuandaa Mazingira mazuri ya Uwekezaji hapa nchini ili Wawekezaji wanaokuja wawekeze katika Mazingira Bora na endelevu.Ameeleza kuwa Miongoni mwa hatua inazochukua ni pamoja na Uimarishaji na Ujenzi wa Viwanja vya Ndege,Bandari na Miundonbinu ya Barabara ili Wawekezaji wawekeze kwa Matumaini na Mafanikio.
Aidha Serikali inaendelea kuchukua hatua maalum za kuondoa Vikwazo mbalimbali katika Uwekezaji kuvutia Wawekezaji ikiwemo kuondoa Urasimu na kuwa na Miongozo na Sera Bora za Uwekezaji hapa nchini.Rais Dkt, Mwinyi amefahamisha kuwa Umoja wa Ulaya Una Mchango Mkubwa na Muhimu kwa Maendeleo na Sekta ya Uwekezaji pamoja na ustawi wa maisha ya Wananchi.
Amebainisha kuwa Uwekezaji wa Ulaya hapa Zanzibar unachangia Asilimia 31 ya Miradi yote ya Uwekezaji iliosajiliwa unaofikia thamani ya Euro Bilionii 2.8 na kutoa fursa za Ajira Elfu 19.Dkt,Mwinyi amezitaja Sekta sita ambazo Serikali imezipa Kipaumbele katika Uwekezaji na kuwakaribisha Wawekezaji kuwekeza.Sekta hizo ni Uchumi wa Buluu, Uvuvi wa Bahari kuu, Utalii alioitaja kuwa Sekta Kuu ya Uchumi wa Zanzibar,Mafuta na Gesi,Kilimo,Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Miundonbinu ya Barabara.
Dkt, Mwinyi amewasisitiza Washiriki wa Kongamano Hilo kulitumia kuwa nyenzo ya kuibua maeneo mapya ya Ushirikiano Baina ya Sekta Binafsi , Serikali na Umoja wa Ulaya na kubaini njia Bora za kutatua Changamoto ziliopo hivi sasa katika Uwekezaji.Rais Dkt ,Mwinyi alishuhudia Utiaji Saini wa Mkataba wa Ushirikiano Baina ya Umoja wa Ulaya na Mamlaka ya Uwekezaji ya Zanzibar (ZIPA) pamoja na kuzindua Ripoti ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya hapa Zanzibar ya Mwaka 2023.