Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imefanya juhudi Maalum za kuhakikisha Bidhaa za Vyakula zinakuwepo za kutosha Wakati wa Ramadhani.Alhaj Dkt, Mwinyi ametoa Tamko hilo alipozungumza katika Kongamano la Kumi la Kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Ukumbi wa Idrissa Abdulwakil Kikwajuni.
Amefahamisha kuwa Serikali imeandaa Mazingira Wezeshi ya Uingizaji wa bidhaa hizo hapa nchini.Ameendelea kuwahimiza Wafanyabiashara kutopandisha bei za bidhaa wakati wa Ramadhani pamoja na kufuata bei Elekezi ili kuwapa Unafuu Wananchi Kumudu Kununua.Akizungumzia Suala la Amani wakati Nchi Ikielekea katika Uchaguzi Mkuu Mwaka huu amewasisitiza Wanasiasa, Viongozi wa Dini na Waandishi wa Habari kupaza Sauti zao kuhubiri Amani ili Nchi iendelee kuwa na Utulivu.
Alhaj Dkt, Mwinyi ameipongeza Jumuiya Ya Zanzibar Welcoming Ramadhan Conference kwa kuandaa Kongamano hilo kwa Mafanikio kwa Miaka Kumi Mfululizo na Kuridhia Ombi la KĖ§ulifanya kuwa la Kimataifa.Wahadhiri Mashuhuri wa Waliwasilisha Mada katika Kongamano hilo zilizoakisi Maadili ya Uislamu wakati wa Ramadhani.
Akiwasilisha Mada ya Umuhimu wa Amani na Utulivu katika Uislamu Sheikh Juma Amiri amewanasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu kuishi kwa Amani na Kuepuka Shari,Mifarakano isio na tija na kusoma Dini kwa Bidii.