Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema jamii ina Wàjibu wa Kujifunza Umuhimu wa Amani kupitia Mambo yanayojiri katika Nchi zilizokosa Amani Ulimwenguni.Akizungumza katika Dua Maalum ya Kuiombea Nchi pamoja na Viongozi Wakuu ,Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan iliofanyika Chaani Tangini, Alhaj Dkt, Mwinyi amesema Amani ni jambo la kwanza kwa Taifa lolote linalohitaji Maendeleo na Maisha Bora ya Watu wake.

Amefahamisha kuwa Watu wanaohitaji Maendeleo na Kuwepo kwa Haki wanapaswa kufahamu kuwa Amani ya Nchi ndio jambo la kwanza linalohitaji kupewa kipaumbele.Rais Dkt, Mwinyi ameeleza kufarijika na Kazi Nzuri inayofanywa na Afisi ya Mufti wa Zanzibar ya Kumaliza Mifarakano katika Taasisi za Kidini ,Miskiti na Madrassa hatua inayochangia kuwepo kwa Amani ndani ya jamii.

Alhaj Dkt, Mwinyi ameendelea kuwahimiza Wanasiasa, Waandishi wa Habari na Viongozi wa Dini kutumia nafasi zao kuhubiri Umuhimu wa Amani.Dkt,Mwinyi amewasisitiza Wananchi kuendelea Kuiombea Nchi Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba na kuwashukuru walioandaa Dua hiyo aliyoielezea kuwa ni zawadi kubwa kwa Mwanaadamu.Baada ya Dua hiyo Alhaj Dkt, Mwinyi aliwaswalisha Waumini wa dini ya Kiislam ya Sala ya Adhuhuri katika Kiwanjani hicho.