Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amekabidhi Sadaka ya Futari kwa Wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Mjini Magharibi.Makabidhiano hayo yamefanyika Viwanja vya Mapinduzi Square Michenzani ambapo Wananchi mbalimbali wamejitokeza kupokea Sadaka Hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo Rais Dkt , Mwinyi amefahamisha kuwa Sadaka Hiyo imetolewa na Mfadhili Nd, Jaffar aliyemkabidhi Dkt Mwinyi Ili kuwagaia Wananchi.Rais amemshukuru Mfadhili Huyo na Wananchi waliojitikeza kuipokea.
Wakati huohuo Rais Dkt, Mwinyi amekabidhi Sadaka Hiyo ya Bidhaa za Chakula kwa Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mjini Magharibi ili Kuendelea na Ugawaji kwa Wananchi katika Wilaya wanazoziongoza.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana amemshukuru Dkt, Mwinyi kwa Kuendeleza Utaratibu huo kila Mwaka kwa Makundi Maalum ya Watu wenye Ulemavu, Yatima , Wajane na Wanaoishi katika Mazingira Magumu.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu Kula Futari ya pamoja.
Wakati huo huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi ameshiriki katika Hafla ya Futari ambayo imefanyika katika Ukumbi wa Idrissa Abdulwakil Kikwajuni ,Wilaya ya Mjini ,Mkoa wa Mjini Magharibi.Akizungumza katika Futari Hiyo Rais Dkt, Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi Kuendelea kuiombea Nchi Amani pamoja na Viongozi Wakuu Ili waendelee kuiongoza Nchi kwa Amani na waendelee kutekeleza Mambo ya Maendeleo.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mke wa Rais wa Zanzibar,Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi.Rais Dkt, Mwinyi amekuwa na Utaratibu huo kila Mwaka unaofanyika katika Mikoa yote ya Zanzibar.