Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaongoza Mamia ya Wana Mazoezi katika Matembezi ya Siku ya Mazoezi Kitaifa Kisiwani Pemba.Matembezi hayo ya Kilomita Tano yalioanzia Kinyasini hadi Uwanja wa Mnazi Mmoja Wete yaliambatana na Mazoezi ya Viungo .
Akizungumza baada ya Kushiriki Mazoezi hayo Rais Dk, Mwinyi amewasisitiza Wananchi kuendelea kufanya Mazoezi ili kuimarisha afya zao na kuepukana na Maradhi yasioambukiza.Rais Dk,Mwinyi ameeleza kuwa Maradhi yasioambukiza ikiwemo Kisukari,Presha, Unene uliokithiri na shinikizo la Moyo yamekuwa Tishio la Kiafya hivi sasa lakini yanaepukika kwa jamii kufanya mazoezi .
Rais Dk, Mwinyi ameihakikishia Zabesa kuwa Serikali itaendelea kuunga Mkono Tamasha hilo na kukipongeza Chama hicho kwa kuiendeleza siku hiyo ya mazoezi ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe mosi Januari ya kila mwaka kwa Mafanikio kwa Miaka 15 na kusisitiza kuwashawishi watu wengi zaidi kufanya Mazoezi.
Akizungumzia Suala la Amani Rais Dk, Mwinyi amewaasa Viongozi wa Dini na Wanasiasa kuhubiri Amani kwa wananchi na kuacha kuhubiri Chuki, Ubaguzi ,Fitna na Mifarakano ya Kisiasa wakati nchi ikielekea katika Uchaguzi Mkuu Mwaka huu.
Akizungumza katika Tamasha hilo Kaimu Waziri wa Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo Lela Muhammed Mussa amempongeza Rais Dk, Mwinyi kwa Hotuba yake ya Kuukaribisha Mwaka Mpya alioielezea kuwa ni Dira ya kuwaongoza Wazanzibari kuelekea Mafanikio ,Umoja na Amani ya Nchi ambazo ndio Tunu za Taifa.
Aidha ameeleza kuwa Maendeleo katika Sekta ya Michezo yanayoendelea nchini yanachochewa na Ujenzi wa Miundombinu ya Michezo ikwemo Viwanja vya Kisasa