Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dkt Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuweka Mkazo wa kuwasaidia Masikini ,Wajane na Yatima ili Kuwapa Unafuu wa Maisha wakati wa kufunga Ramadhani.Alhaj Dkt, Mwinyi ametoa Tamko hilo alipotoa Salamu kwa Waumini wa Masjid Hamieni Muyuni C ,Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kujumuika katika Dua Maalum ya Kuwaombea Viongozi Wakuu wa Nchi na Sala ya Ijumaa.
Amefahamisha kuwa Jamii ina Wajibu Mkubwa wa Kuyasaidia Makundi hayo Maalum kwani ni thawabu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu ili nao wafunge kwa Utulivu.Amewakumbusha Wafanyabiashara kutopandidha Bei za Bidhaa za Vyakula wakati wa Ramadhani ili Wananchi Wamudu kununua bidhaa hizo.
Alhaj Dkt,Mwinyi ameeleza kuwa Ramadhani ni wakati Muhimu kwa Watu Kuhurumiana na kujenga Uhusiano Mwema na Wengine pamoja na kumcha Mungu kwa bidii.Akizungumzia suala la Amani Alhaj Dkt ,Mwinyi amewanasihi Wanasiasa, Viongozi wa Dini na Waumini kwa Ujumla kulichukua suala la Amani kuwa Agenda namba moja katika hutuba zao ili Nchi iendelee kuwa na Amani.
Akizungumzia suala la Malezi Alhaj Dkt, Mwinyi amehimiza kwa Vijana Kuelimishwa Elimu ya Dini na kutoa rai kwa Miskiti na Madrrasa kutekeleza Wajibu huo.Alhaj Dkt, Mwinyi amewahakikishia Wananchi wa Mkoa wa Kusini kuwa Serikali inatekeleza Miradi Mikubwa ya Kimkakati ya Maji na Umeme yenye lengo la kumaliza kabisa Matataizo katika Maeneo mbalimbali hapa nchini.
Naye Khatibu wa Masjid Hamieni Khatibu Ali amewanasihi Waumini wa dini ya Kiislamu Kutenda Mema na kuzishukuru Neema za Mwenyezi Mungu wakati huu wa kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.Akitoa Salamu za Wananchi Sheikh Ramadhan Rajab amempongeza Rais Dkt, Mwinyi kwa Utekelezaji wake wa Vitendo na kuahidi kuunga Mkono Maono yake ya Kimaendeleo.