Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Viongozi wa Dini, Wanasiasa na Waandishi wa Habari kutumia Majukwaa yao Kutoa Kauli nzuri zenye Kuleta Umoja ndani ya Jamii na Amani ya Nchi.Alhaj Dk, Mwinyi ametoa tamko hilo alipotoa Salamu Kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi alipojumuika kwa Sala ya Ijumaa.

Alhaj Dk, Mwinyi ameeleza kuwa Viongozi wa Dini na Wanasiasa Wawe na kauli zenye kusikilizwa na Watu wengi hivyo ni Vema wakatumia Majukwaa yao kutoa Kauli njema zitakazojenga Umoja ,Undugu, Mshikamano na Amani.“Kauli zenu ni muhimu sana ,Mtusaidie kuhimiza Amani na Umoja ndani ya Jamii” alisema Dk,Mwinyi.

Akiwazungumzia Waandishi wa Habari Alhaj Dk, Mwinyi amewahimiza kutumia Kalamu zao vizuri na kujihadhari na yale wanayoyaandika katika Televisheni ,Redio na Mitandao ya Kijami kuwa hayana Viashiria vya Uvunjifu wa Amani.Alhaj Dk ,Mwinyi amefahamisha Kuwa Kwa miaka Mingi iliopita Uzoefu Umeonesha Kuwa Zanzibar ilikuwa ikiingia katika Mifarakano kila Unapofika Wakati wa Uchaguzi jambo lisilopaswa kutokea tena.

Aidha Alhaj Dk, Mwinyi ameeleza kuwa ni Lazima Nchi ioneshe kuwa Inaweza kufanya Uchaguzi kwa Amani hatimae Ipige hatua Zaidi za Maendeleo.“Hilli ndilo litakalotupa yale yote tunayoyataka yakiwemo Maendeleo katika Nyanja yoyote ile” alisisitiza Dk,Mwinyi.