RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Viongozi, mashekhe na Waumini wa dini ya kiislamu kuendelea kuhubiri Amani Maadili na tabia njema ili kujenga Jamii Bora.Alhaj Dk.bMwinyi ameeleza kuwa ni majukumu la kila mmoja kusisitiza jambo hilo na wala sio la kuwaachia Masheikh na Maamiri pekee yao.
Ametoa tamko hilo alipofungua Ijitimai ya sita, Msikiti wa Fissabililah Tabligh Markaz, Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.Aidha, Alhaj Dk. Mwinyi amewahimiza Masheikh kutumia mikusanyiko ya Kiimani kuiombea nchi Amani ili ili Serikali iendelee na mipango ya Maendeleo.
Alhaj Dk. Mwinyi ameeleza kuwa bila ya kuwepo Amani hakuna jambo linaloweza kufanyika na kufikia malengo ya nchi. Ametoa wito kwa wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali za kuleta Maendeleo katika sekta tofauti ili nchi ipate mafanikio zaidi.Rais Alhaj Dk. Mwinyi ameipongeza Jumuiya ya Fissabilillah Tabligh Markaz kwa kuuendeleza Ijitimai kwa mafanikio makubwa kila mwaka na kuahidi kwa Serikali kuunga Mkono.
Aidha, ameielezea Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kuwa kiungo muhimu kwa Serikali katika kusimamia masuala ya dini ya Kiislamu.
Akitoa salamu Makamu Amir Mkuu wa Fissabilillah Tabligh Markaz Afrika Mashariki, Amir Almas Abdalla ameelezea mafanikio ya Zanzibar yanatokana na kuwa na Kiongozi Mwenye moyo wa huduma kwa wananchi anaowaongoza.
Amewanasihi Viongozi wa dini kutojiingiza kwenye Siasa na mambo yalio nje ya misingi ya uislamu.
Akitoa salamu za Jumuiya ya Kiislamu za Fissabilillah Tabligh Markaz, Zanzibar Sheikh Kassim Saleh ameielezea hali ya Amani ya nchi na kasi ya Maendeleo iliyofikia Zanzibar zinatokana na kuwa na Rais mcha Mungu na anaejali watu wake.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti wa Zanzibar, Sheikh Khalid Mfaume amesema kutokana na kuwepo kwa mambo mengi mabaya katika jamii ni lazima kuwepo kundi la kuwakumbusha Waumini kutenda mema na kusisitiza kwa Masheikh kutumia Ijitumai kuhubiri maadili mema , amani, umoja na upendo.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti wa Zanzibar, Sheikh Khalid Mfaume amesema kutokana na kuwepo kwa mambo mengi mabaya katika jamii ni lazima kuwepo kundi la kuwakumbusha Waumini kutenda mema na kusisitiza kwa Masheikh kutumia Ijitumai kuhubiri maadili mema , amani, umoja na upendo.