Benki ya Dunia Imeipatia Zanzibar Kiasi cha Dolla Milioni 100 kwa ajili kuimarisha Miundombinu ya Sekta ya Afya hapa nchini.Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Mwa Afrika Milena Stefanova ametoa Tamko hilo alipozungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Benki ya Dunia kwa Msaada huo aliouelezea kuwa umekuwa Kichocheo cha Mabadiliko makubwa na kuimarika kwa Miundombinu ya Matibabu.

Amefahamisha kuwa licha ya Serikali kufanikiwa kujenga Hospitali za Wilaya na Vituo vya Afya bado zipo Changamoto zinazohitaji Utatuzi wa haraka na kuiagiza Wizara ya Afya kutumia fedha hizo vizuri kwa kuimarisha Miundimbinu ya Afya Mafunzo kwa Watendaji na Upatikanaji wa Vifaa vya Kisasa vya Matibabu

Dkt, Mwinyi na ameuelezea Ujumbe huo kuwa Serikali ina Malengo Mahsusi ya kuifanya Zanzibar kuwa kituo Bora cha Matibabu kwa Nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa Ujumla na kuipongeza Benki ya Dunia kwa kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.

Rais Dkt,Mwinyi ameishauri Wizara ya Afya kufanya kazi kwa Ukaribu na Mtaalamu wa Ubunifu wa Miundonbinu ya Matibabu wa Benki ya Dunia Profesa Francis Kere kutafuta Wakandarasi wazuri na Weledi kusimamia Ujenzi wa Miundombinu ya Matibabu ili Msaada huo wa fedha Utumike kwa kwa Ufanisi na kuleta Mabadiliko yanayostahiki katika sekta

Naye Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Kusini Mwa Afrika Milena Stefano ameeleza kuwa Benki hiyo inaridhika na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Zanzibar za kuimarisha huduma za Afya na kuahidi kuendelea na misaada kwa ustawi wa watu wake.

Akizungumza katika hafla Hiyo Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazroui ameeleza kuwa Wizara hiyo inajipanga vema kuhakikisha fedha hizo zinaenda kutumika kufanikisha lengo la kuifanya Zanzibar kuwa kituo cha pekee cha Utalii waTiba na Matibabu na Mafunzo ya Afya ( HEALING ISLAND)kama zilivyo nchi za India na THailand.