Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk, Hussein Ali Mwinyi amewanasihi Waumini wa Dini ya Kislamu Kuitumia Misikiti Vizuri Kukabiliana na Changamoto Katika jamii.Alhaj Dk, Mwinyi ametoa Tamko hilo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Ibada ya Sala ya Ijumaa na Kuufungua Msikiti Mpya wa Chanjaani Mwanamashungi ,Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.

Alhaj Dk, Mwinyi amefahamisha kuwa ni vema Misikiti Ikatumika kwa Kusali , Kusoma Pamoja na kuitunza ili iwe na Mazingira mazuri kwa Ibada.Aidha amesisitiza kwa Waumimi kuweka mkazo katika Kusoma na kutoa Elimu ya dini kwa dhamira ya kunusuru jamii na Changamoto za Kijamii.

Akizungumzia Suala la Amani Alhaj Dk, Mwinyi amewahimiza Waumini wa dini ya Kislamu,Viongozi wa Dini na Wanasiasa pamoja na Waandishi wa habari Kuhubiri Amani zaidì wakati nchi ikielekea katika Uchaguzi Mkuu.

Naye Khatibu wa Msikiti wa Chanjaani Mwanamashungi Sheikh Hassan Suleiman amesema suala la kuimarisha Misikiti ni jambo jema na ni Jukumu la Waumini waliomuamini Mwenyezi Mungu.Aidha amewanasihi Waumini wa dini ya Kiislamu kufahamu nafasi Misikiti ya kuisaidia Jamii hususan Makundi Maalum ya Mayatima na Wajane .

Katibu Mtendaji wa Afisi ya Mufti Sheikh Khalid Ali Mfaume amewasisitiza Waumini wa dini ya kislamu Kuwa na Utaratibu wa Kutoa Sadaka kwani kuna Manufaa makubwa kwa kila Muumini.