State House Blog

Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akipokea salamu ya heshma ya gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma katika kilelel cha maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanziibar.
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akikagua Gwaride la heshma la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sherehe zilizofanyika Mkoani Dodoma
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Sera Bunge,Kazi, Vijana,Ajira na Walemavu Jenesta Joakim Muhagama wakatri alipowasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Dkt.Akinumwi Adenisa mara baada ya kumalizika kwa sherehe za madhimisho ya kilele miaka 54 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika mapokezi yake mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mkoani humo,ambapo anatarajiwa kushiriki katika sherehe za maadhimishi ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanzania zitakazofanyika,katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Dkt. Bilinith Mahenge mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mkoani humo,ambapo anatarajiwa kushiriki katika sherehe za maadhimishi ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanzania zitakazofanyika,katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma