State House Blog

Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokewa na mamia ya wananchi na Wanachama wa CCM Zanzibar.

  • Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk , Hussein Ali Mwinyi akivishwa shada la maua wakati alipowasili katika kiwanja cha Ndege cha Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Dodoma alipoteuliwa Kupeperusha Bendera ya Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu Ujao katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Uliofanyika hivi Karibuni.
  • Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk , Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na wanachama wa chama cha Mapinduzi,wananchi pamoja na wanafunzi mbali mbali waliojipanga pembezoni mwa barabara kwa ajili ya kumlaki baada ya kutoka mjini Dodoma alipoteuliwa kugombea Urais wa zanzibar kwa mara ya pili mfululizo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
  • Wanafunzi mbali mbali waliofika kumlaki Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi akitokea Jijini Dodoma ambapo ameteuliwa kugombea nafasi hiyo.
  • Wanachama wa chama cha Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika kiwnja cha ndege cha Abeid Amani Karume Zanzibar wakimlaki Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi alipowasili katika kiwanja hicho akitokea jijini Dodoma ambapo amaeteuli kugombea nafasi hiyo.
  • Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Mheshimiwa Idrisa Kitwana Mustafa akitoa salamu zake za Mkoa kwa Mheshimiwa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ambae pia na mgombea wa Urais wa zanzibar kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi Zanzibar hapo katika viwanja vya Kisonge Michezani zanzibar.
  • Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk , Hussein Ali Mwinyi akiwa katika gari la wazi akiwasalimia wananchi waliofika kumpokea kando kando mwa barabara ya kutokea Uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume jijini Zanzibar akitokea Jijini dodoma ambapo ameteuliwa kuipeperusha bendera ya Chama cha mapinduzi kwa upande wa Zanzibar.