Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Mwinyi amewaapisha Viongozi aliowateuwa hivi karibuni.Hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Zanzibar.
14 Nov 2024
11
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisaini hati ya kiapo ya Ndg.Hiji Dadi Shajak,baada ya kumuapisha kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar,hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 14-11-2024 na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said
MHE Iddi Said Khamis akisaini hati ya kiapo baada ya kumaliza kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi,kuwa Kadhi wa Mahkama ya Kadhi ya Rufaa Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 14-11-2024 na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg.Hiji Dadi Shajak,kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 14-11-2024 na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said
VIONGOZI Wateule walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk .Hussein Ali Mwinyi, wakiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar wakipitia hati zao za kiapo kabla ya kuapishwa leo 14-11-2024 (kushoto ) Mhe. Iddi Said Khamis, ameteuliwa kuwa Kadhi wa Mahkama ya Kadhi ya Rufaa Zanzibar na Ndg. Hiji Dadi Shajak, ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Iddi Said Khamis kuwa Kadhi wa Mahkama ya Kadhi ya Rufaa Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 14-11-2024 na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said
Rais wa Zanbzibar amezungumza na Uongozi wa Benki ya Stanbic Tanzania Ikulu Zanzibar.
13 Nov 2024
10
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk .Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Stanbic Tanzania Patrick Rutabanzibwa, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-11-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Stanbic Tanzania Patrick Rutabanzibwa (kulia kwa Rais) akiongoza Ujumbe wa Uongozi wa Benki hiyo, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 13-11-2024